[metaslider id=”4631″]
Watafiti kutoka Taasisi Ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA wamefanya ziara katika Bandari Ya Kemondo Mkoani Kagera ikiwa ni muendelezo wa ziara ya kutafuta maendeo ya kufanyia tafiti katika mikoa ya kanda ya ziwa.
Watafiti hawa walipokelewa na Afisa wa Bandari ya Kemondo Bw. Titus Majula na kupewa historia fupi ya bandari ya Kemondo na shughuli mbalimbali zinazofanya na wananchi wanaoishi maeneo ya karibu na bandari. Bandari ya Kemondo ndio bandari kubwa kuliko zote katika ziwa Victoria ikiwa na ukubwa hekeri 126
Aidha bw. Titus Majula amesema licha ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanyika katika bandari ya kemondo kumekuwa na changamoto ya viumbe wa haribifu kama Popo kuharibu mazao mbalimbali ya wananchi wa Kemondo na Kisiwa cha Kishaka.
Bw. Majula amesema “ Popo wamekuwa ni tatizo kubwa sana katika eneo hili la kemondo na visiwa vyake wamekuwa wakiharibu mazao shambani kama vile ndizi na parachichi. Tunashukuru watafiti kututembelea najua mtatusaidia mbinu za kuwadhibiti hawa popo”
Prof. Apia Massawe na Prof. Mulungu wamehaidi kurudi katika Wilaya ya Kemondo kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na viumbe hai waharibifu ili kuisaidia jamii kuondokana na matatizo yanayosababishwa na viumbe hivyo.