Wadau kutoka Wizara ya Afya watembelea Taasisi yetu tarehe 16 July 2021.
Lengo kuu ni kuendelea kudumisha uhusiano na kushirikiana katika teknolojia ya Panyabuku kwenye kubaini vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Katika mazungumzo hayo Wizara imeahidi kufuatilia agizo la Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Abel Makubi alilotoa tarehe 26 Februari 2021 alipotembelea mradi wa Panya dhidi ya kuongeza vituo vinavyotumia huduma ya teknolojia ya Panya kwenye unusaji wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini.
Pia, wadau hao wametoa pole kwa kumpoteza Mtafiti Mwandamizi na Mkuu wa Mradi, Dkt. Georgies Mgode na kuhakikisha kuendeleza ushirikiano kati ya Wizara, Asasi ya Apopo na Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu, Dkt. Ladslaus Mnyone amefurahishwa sana na ziara na kuahidi ushirikiano madhubuti ili kuendeleza teknolojia lengwa kwa manufaa ya kitaifa na dunia kwa ujumla.