Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibufu SUA (IPM) inashiriki maonesho ya wakulima kanda ya mashariki katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere vilivyopo mkoani Morogoro.
Maonesho haya ya wakulima yaliyobeba kauli mbiu isemayo “Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”. Lengo la kauli mbiu hii ni kuhamasisha ushiriki wa vijana na wanawake katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, Ufugaji wa mifugo na uvuvi .Hii ni kutokana na ukweli kwamba Vijana na wanawake ndio kundi kubwa sana katika jamii ya kitanzania. Kundi hili litajikita katika uzalisha chakula litaleta mafanikio makubwa kupitia kupitia klimo, ufugaji na uvuvi Tanzania.
Katika maonesho haya Mgeni rasmi siku ya ufunguzi alikuwa Waziri Mkuu mstaafu awamu ya nne Mhe. Mizengo Peter Pinda ambapo aliweza kupata wasaa wa kutembelea mabanda ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo. Akiwa katika mabanda ya SUA aliweza pia kutembelea Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibu ikiwemo APOPO kuona teknolojia mbalimbali zinazotumika kudhibiti viumbe hai waharibifu mashambani na majumbani Pamoja na kusaidia kuokoa Maisha ya jamii.
Miongoni mwa teknolojia zinazooneshwa ni kama zifuatazo;-
i. Teknolojia ya udhibiti wa panya kwenye mashamba ya Mpunga
ii. Teknolojia ya matumizi ya ndege aina ya bundi kupunguza panya waharibifu kwenye mashamba
iii. Matumizi ya mitego mbalimbali kudhibiti panya ndani ya nyumba
iv. Matumizi ya viuatilifu vya kuua panya majumbani
Aidha kwa upande wa APOPO mgeni rasmi aliweza kuona jinsi panya wanavyotumika kusaidia jamii katika mambo mbalimbali kama vile Kutambua vimelea vya kifua kikuu kwenye makohozi ya binadamu na jinsi panya wanavyotumika kutambua harufu za milipuko ya mabomu.
Maonesho haya yalianza tar 1-8-2023 yanaendelea hadi tar 8-8-2023 Karibuni sana katika banda la Taasisi ya Udhibiti wa Viumbe Hai Waharibifu.