Watafiti wa kituo cha kudhibiti viumbe hai waharibifu (SUA) Prof.Apia Massawe na Prof Loth Mulungu watoa mafunzo ya udhibiti wa panya katika mashamba ya mpunga Kijiji cha Mkula kilichopo wilayani Kilombero mkoani Mororgoro.
Mafunzo haya yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi ya kijiji cha mkula na wakulima wa mpunga katika bonde la mkula.
Mafunzo haya yamekuja baada ya watafiti kubaini njia mbadala ambayo itawasaidia wakulima katika mapambano ya panya waharibifu wa mazao mbalimbali shambani kwa gharama nafuu kwa usalama wa afya ya wakulima na walaji.
“Wakulima wengi wamekuwa na changamoto ya mazao yao kuharibiwa na panya na wakulima wengine kutumia njia mbalimbali kudhibiti panya bila mafanikio.Kwa kutumia njia hii ya TBS(Trap barrier system) tunaweza kuondokana na tatizo la mazao kuharibiwa na panya shambani na kuweza kupata mazao mengi na kukuza uchumi wetu pia” amesema Prof Mulungu
Wakulima alipata fursa ya kuuliza maswali watafiti na kupatiwa majibu ya kuridhisha kuhusu namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu mashambani.