TANGAZO
Mkurugenzi wa kituo cha utafiti na udhibiti wa viumbe hai waharibifu (SUA Pest Management Centre) kilichopo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro, anawatangazia kuwa kituo kinatoa fursa ya wabunifu wa Teknolojia mbalimbali za udhibiti wa viumbe hai waharibifu kuonana na watafiti wake.
Teknolojia inayokidhi vigezo, itafanyiwa majaribio ya Kisayansi kwa lengo la kuhakiki ufanisi,kuboresha na kuunganishwa na wenye viwanda.
Zoezi hili limeanza kuanzia tarehe 1 / 12/ 2019 hadi tarehe 30 /1/2020.
Mhusika anatakiwa awe na Teknolojia bunifu ya kudhibiti viumbe hai waharibifu kama vile Panya, Mende, Kunguni, Viroboto, Mbu, Dumuzi n.k
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi sasa kwa anuani zifuatazo;
Simu: 0623-125990
au fika moja kwa moja kituoni kwetu campus kuu SUA