Mbali na mtazamo hasi wa jamii hasa ya kitanzania uliopo kwa ndege aina ya Bundi, Kituo Cha Kudhibiti Viumbe Hai Waharifu kimekuja na mtazamo chanya kupitia tafiti zake zinazofanywa dhidi ya ndege aina ya bundi. Bundi ni aina ya ndege ambao upendelea kuwinda wanyama wadogo wadogo kama Panya, wadudu na hata ndege wengineo hasa nyakati za Usiku.
Tafiti zinaonesha kuwa Bundi mmoja ana uwezo wa kula zaidi ya Panya kumi (10) kwa siku moja, na pia kuna baadhi ya bundi huishi kwa makundi na kuwinda kwa pamoja, hivyo ndani ya msimu mmoja kundi moja la bundi linaweza kula mamia ya panya wadogo na kupunguza athari za uharibifu wa mazao unaosababishwa na Panya shambani.
[metaslider id=”4139″]
Mkulima anahitaji sana aina ya ndege bundi ndani ya shamba lake kama njia asili ya kupunguza kiwango cha viumbe hai waharibifu wakiwemo Panya waliopo katika shamba lake. Hivyo Mkulima anatakiwa kutengeneza mazingira mazuri kwa lengo la kuvutia aina ya ndege hao hasa kwa kufanya yafuatayo;
- Kujenga viota (visanduku) ambavyo vitatumika kama sehemu ya kuishi Bundi na kuvining’iniza kwenye miti au nguzo ndani ya shamba.
- Kuweka nguzo au miti ndani ya shamba kwaajili ya kuwezesha bundi kusimama hasa wakati wa mawindo yake.
Rejea kwenye mitandao yetu ya kijamii na pia endelea kutembelea tovuti yetu ili kuweza kuhabarika zaidi na tafiti zetu zinazoendelea hapa kituoni.