[metaslider id=”4753″]
Watafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu SUA wamefanya ziara ya kiutafiti katika Zanzibar ili kuangalia na kuidhinisha maeneo mapya ya Utafiti wa matatizo yanayosababishwa na panya.
Watafiti hao Prof. Apia Massawe na Prof. Loth Mulungu wametembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibari (ZARI) lengo kuu likiwa ni kukutana na watafiti wa taasisi hiyo na kujadiliana namna ya kushirikiana kufanya kazi kwa pamoja ili kuwasaidia wakulima Zanzibar.
ZARI ni Taasisi inayojishughulisha na tafiti za kilimo katika kisiwa cha Zanzibar ikijihusisha na utafiti wa wadudu waharibifu wa mazao shambani kama vile Nzige, viwavi jeshi na wengineo. Katika kupanua wigo wa tafiti hizi watafiti kutoka ZARI wamefurahishwa na ujio wa watafiti kutoka Taasisi ya Kudhibiti Viumbe Hai Waharibifu kuweza kushirikiana nao katika tafiti mbalimbali.
Aidha Prof. Apia Massawe ameelezea Shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kituo Cha Umaahili cha Afrika cha Kutafiti Mbinu na Tekinologia za Kudhibiti Panya ikiwa ni pamoja na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu.Pia amesema itakuwa ni ushirikiano mzuri kwa upande wa wanafunzi wa shahada ya Uzamili wanaofanya tafiti zao mikoani wa Unguja na Pemba.
Watafiti hao Prof. Apia Massawe na Prof. Loth Mulungu wamesema ziara hii imelenga katika kutimiza yafuatayo
- Kutafuta maeneo ambayo yanafaa kufanyia tafiti mbalimbali zinazohusu ikolojia ya panya kwenye sehemu tofauti huko Zanzibar,
- Kuidhinisha maeneo ya tafiti kuhusiana na panya wanaopatikana kwenye mikoa tofauti Zanzibar,
- Kuangalia mazingira asili kama misitu, vichaka, maeneo ya miinuko na ya tambarare ambayo yanaweza kufanyiwa utafiti ili kugundua aina mpya za panya
- Kujionea maeneo yanayotumika kwa shughuli za binadamu kama kilimo na ufugaji ambapo kunatokea milipuko ya panya ili kugundua aina ya panya waliopo na kinachosababisha milipuko hiyo
- Kufanya utafiti juu ya magonjwa yanayobebwa na kusababishwa na panya kwa binadamu, n.k